Sera ya Faragha
Ilisasishwa mara ya mwisho: Julai 2026
Sera hii inaeleza jinsi Lumenlabs ("sisi") inavyokusanya, kutumia na kulinda taarifa unapotumia DukaPOS (programu ya mauzo) au tovuti ya lumenlabs.co.tz.
1. Taarifa Tunazokusanya
- Taarifa za akaunti: jina la duka, barua pepe au namba ya simu, nywila (iliyosimbwa/hashed).
- Taarifa za biashara unazoingiza mwenyewe: bidhaa, mauzo, wateja wa mkopo (madeni), akaunti za fedha, matumizi.
- Taarifa za kifaa: "device token" inayotambulisha simu/tableti yako ndani ya mfumo.
- Data ya kiufundi ya msingi (kama muda wa mwisho kutumia mfumo) kwa ajili ya utendaji na usalama.
2. Jinsi Tunavyotumia Taarifa
Taarifa zako zinatumika pekee kuendesha huduma ya DukaPOS kwa duka lako: kusawazisha mauzo kati ya vifaa vyako, kutengeneza ripoti zako, na kukusaidia wakati unapohitaji msaada. Hatuuzi taarifa zako kwa kampuni nyingine.
3. Ugawaji wa Taarifa (Tenant Isolation)
Data ya kila duka imetengwa kwenye hifadhidata yetu — duka lingine haliwezi kuona bidhaa, mauzo au wateja wa duka lako. Hii inatekelezwa ngazi ya hifadhidata (database-level row security), si tu ndani ya programu.
4. WhatsApp na Huduma za Nje
Ukichagua kutuma risiti kupitia WhatsApp, maandishi ya risiti hufunguliwa kwenye WhatsApp yako mwenyewe kutumwa — hatutumi taarifa za mauzo kwa WhatsApp/Meta bila wewe kuchagua kufanya hivyo.
5. Uhifadhi wa Data (Backups)
Tunafanya nakala za hifadhidata (backups) mara kwa mara kuzuia upotevu wa data. Tunaendelea kuboresha usalama wa nakala hizi (ikiwemo kuzihifadhi nje ya seva kuu na kuzisimba/encrypt).
6. Haki Zako
Unaweza kuomba nakala ya taarifa zako, kuomba zifutwe, au kufunga akaunti yako wakati wowote kwa kuwasiliana nasi (maelezo hapa chini).
7. Wasiliana Nasi
Maswali kuhusu sera hii au taarifa zako: WhatsApp +255 62 121 9695 au barua pepe nelson@lumenlabs.co.tz.