Vigezo na Masharti
Ilisasishwa mara ya mwisho: Julai 2026
Kwa kutumia DukaPOS unakubaliana na masharti haya. Tafadhali yasome kwa umakini.
1. Akaunti Yako
Wewe ndiye unayehusika na usalama wa akaunti yako, ikiwa ni pamoja na nywila yako na "device token" za vifaa vyako. Usiruhusu mtu asiyeaminika kutumia akaunti yako.
2. Mipango na Malipo
- Mpango wa Kuanza (bure): hadi bidhaa 100, bila malipo.
- Mpango wa Biashara: TZS 15,000 kwa mwezi, baada ya kipindi cha majaribio cha siku 14 bila malipo.
- Unaweza kusitisha (cancel) mpango wa Biashara wakati wowote; hutalipishwa tena baada ya kusitisha.
- Bei zinaweza kubadilika; tutakujulisha kabla ya mabadiliko yoyote kuathiri akaunti yako.
3. Matumizi Yanayoruhusiwa
DukaPOS ni kwa ajili ya kuendesha biashara halali. Haturuhusu matumizi ya mfumo kwa shughuli haramu, udanganyifu, au kuvunja mifumo yetu ya usalama.
4. Upatikanaji wa Huduma
Tunafanya kazi kwa bidii kuweka mfumo ukifanya kazi muda wote, lakini hatuhakikishii huduma bila makosa au kukatika kabisa (hakuna dhamana rasmi ya SLA kwa sasa). DukaPOS inafanya kazi hata bila mtandao kwenye kifaa chako na kusawazisha data mtandao ukirudi.
5. Wajibu Wetu na Kikomo cha Dhima
Tunajitahidi kulinda data yako kama ilivyoelezwa kwenye Sera ya Faragha. Hata hivyo, kwa kadiri sheria ya Tanzania inavyoruhusu, Lumenlabs haitawajibika kwa hasara zisizo za moja kwa moja zitokanazo na matumizi ya mfumo.
6. Mabadiliko ya Masharti
Tunaweza kusasisha masharti haya mara kwa mara. Mabadiliko makubwa tutayaeleza kwenye ukurasa huu.
7. Sheria Inayotumika
Masharti haya yanaongozwa na sheria za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
8. Wasiliana Nasi
Maswali kuhusu masharti haya: WhatsApp +255 62 121 9695 au barua pepe nelson@lumenlabs.co.tz.